Dar es salaam, sasa unaweza kupata usafiri wa bajaji ukiwa na uberPOA kwenye simu yako
23 Machi 2018 / Tanzania
Sasa unaweza kupata usafir nafuu zaidi muda wowote, wakati wowote kwa kuagiza uberPOA kupitia app yako ya Uber.
Tunataka kurahisisha safari zote za ndani ya Dar Es Salaam, ndio maana tunawaletea uberPOA, usafiri wa bajaji kwa watumiaji wote wa Uber ndani ya Dar Es Salaam.Tuna furaha kuwaletea huduma ambayo inaendana na utamaduni wetu hapa Dar Es Salaam, ikiongezewa na faida ya kupatikana kiganjani mwako.Ukiwa na uberPOA hauna shida ya kusimamisha bajaji njiani. Ni rahisi sana nenda kwenye application ya Uber, andika unapoelekea, halafu chagua uberPOA. Popote pale ulipo bajaji itakufikia ndani ya dakika chache tu. Gharama za usafiri zinaanzia TZS 2,000 tu.
uberPOA itakua pamoja na uberX kwenye app yako na chaguo hili litaonekana maeneo ambayo uberPOA itakua inafanya kazi.
Unapata shida kuiona uberPOA kwenye app yako ya uber?
Kwa sasa uberPOA itapatikana kwa baadhi ya maeneo Dar Es Salaam . Kwahiyo unaweza kuchukuliwa na kushushwa kwenye maeneo ambayo uberPOA inafanya kazi na sio nje ya hapo. Baadhi ya maeneo ambayo uberPOA itafanya kazi ni Mwenge, Sinza, Kijitonyama, Mikocheni A, Mwananyamala, Kinondoni, Namanga, Msasani, Oysterbay, Masaki & Kigamboni. Tutaongeza maeneo ikiwezekana ili kuhudumia watu wengi zaidi.
uberPOA itafuata vigezo na masharti ya usafir ndani ya Dar Es Salaam, hivyo haitabeba wala kushusha mtu sehemu amabyo bajaji haziruhusiwi na mamlaka ya mji.
Gharama za usafiri wa uberPOA zitakua kama ifuatavyo;
- Bei ya chini – TZS 2,000
- Ada ya kughairisha safari – TZS 2,000
- Bei ya kuanzania – TZS 1500
- Bei kwa kilometa – TZS 400
- Bei kwa dakika – TZS 80
Jinsi ya kuagiza usafiri
- Fungua app yako, andika unapoelekea, hakikisha ni katika sehemu ambayo bajaji zinaruhusiwa.
- Chagua uberPOA kwa chini kwenye app yako.
- Bonyeza “confirm uberPOA”
- Na uberPOA yako itakufikia
Waambie uwapendao kuhusu huduma hii!
Waambie marafiki zako juu ya uberPOA na jinsi safari yako ilivyokua kwa kutumia hashtag #uberPOA kwenye Facebook, Twitter na Instagram.
Tafadhali ijulikane ya kwamba maombi yatakuwa ni mengi, kwahiyo endelea kuagiza ukikosa kwa mara ya kwanza
Hujaona uberPOA kwenye app yako? Usihofu, tunazidi kuongeza maeneo ya kufanyia kazi itakapowezekana ili kuhudumia watu wengi zaidi
Dar Es Salaam Team.
Posted by Uber Editor
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Get a trip when you need one
Start earning in your city
Related articles
Most popular
Shinda Vocha za KFC na PizzaHut ukitumia App ya Uber
Pata 10% ya nauli yako ukilipia safari za Uber kwa TigoPesa!

Heshima ni kwa pande zote mbili
