Uanuwai, usawa na ujumuishaji
Kuunda timu zenye vipaji ili kuwahudumia watu kwenye jukwaa tofauti
Kwenye tovuti ya Uber, idadi kubwa ya watu tofauti hutumia safari zetu milioni 30 kwa siku. Tunapoonesha uaunuwai wa kipekee wa watu wanaojiunga kwenye mfumo wetu, tunafanya maamuzi na kutoa bidhaa bora zinazofaidi ulimwengu. Watu tofauti huwaza tofauti. Watu wenye vipaji bora wanaoleta hoja, utambulisho, asili, uzoefu na elimu mbalimbali hutuwezesha kujenga bidhaa zetu na kufanya biashara yetu kwa njia ambayo hutumikia vyema jumuiya mbalimbali zinazotumia bidhaa zetu.
Tunajitahidi kusitawisha mazingira ambayo kila mtu anahisi kuwa anahusika na anaweza kuchangia mafanikio yetu ya pamoja.
Jumuiya ya Uber kwa ajili ya watu wa imani na tamaduni anuwai za kiroho
Jumuiya ya Uber kwa ajili ya wafanyakazi na washirika wa Kihispania na Amerika Kusini
Ripoti za kila Mwaka za Watu na Utamaduni
Kila mwaka, tunachapisha Ripoti yetu ya Watu na Utamaduni ili kushiriki mtazamo wetu wa usimamizi wa mtaji wa binadamu; uanuwai, usawa, ujumuishaji na utamaduni. Tunashiriki takwimu zilizosasishwa za uwakilishi na kuonyesha jinsi tunavyoendelea dhidi ya malengo yetu ya matarajio. Ripoti hiyo ni sehemu muhimu ya mbinu yetu ya kuongeza uwazi kuhusu takwimu za wafanyakazi wetu na mazoea ya mtaji wa binadamu.
Uber inachukua hatua ya kutoa huduma sawa zaidi kwa kila mtu tunayemhudumia. Ili kusimulia hadithi hii vyema, tumeunda mtazamo kamili wa jinsi Uber inavyoleta matokeo kwa kujumuisha Ripoti yetu ya Watu na Utamaduni na Ripoti yetu ya ESG (mazingira, jamii na utawala) ili iwe Ripoti yetu mpya ya Mazingira, Jamii na Utawala.
Kuwa mwajiri wa fursa sawa
Ripoti ya EEO-1, pia inajulikana kama ripoti ya taarifa ya mwajiri, imepewa mamlaka na serikali ya shirikisho ya Marekani na inahitaji kampuni kuripoti takwimu za ajira kulingana na mbari/kabila, jinsia na aina ya kazi.
Ripoti hii inatumiwa kufuatilia na kupima uanuwai, ujumuishaji na usawa kwa wafanyakazi wetu wote, kimsingi ni picha ya wafanyakazi wa Uber nchini Marekani kwa wakati mahususi. Kukuza mahali pa kazi penye wafanyakazi wa aina mbalimbali husaidia biashara yetu kufikiria kwa makini kuhusu malengo yake kulingana na mkakati wetu mpana wa DEI. Tunachagua kufanya ripoti hii ipatikane kwa umma kama sehemu ya ahadi yetu inayoendelea ya kuongeza uwazi na maelezo ya kina kuhusu takwimu za kidemografia za wafanyakazi wetu.
Ripoti ya 2023 EEO-1
Ripoti ya EEO-1 ya mwaka 2022
Ripoti ya EEO-1 ya mwaka 2021
Ripoti ya EEO-1 ya mwaka 2020
Ripoti ya EEO-1 ya mwaka 2019
Kama mkandarasi wa serikali kuu, Uber inajivunia kuwa mwajiri wa fursa sawa/anayepinga ubaguzi. Waombaji wote wa kazi wanaofuzu watazingatiwa kwa ajira bila kuzingatia jinsia, utambulisho wa kijinsia, mwelekeo wa kingono, mbari, rangi, dini, asili ya kitaifa, ulemavu, hadhi inayolindwa ya kustaafu kwa mwanajeshi, umri au sifa nyingine yoyote inayolindwa na sheria. Aidha, tunazingatia waombaji wa kazi wanaofuzu bila kujali historia ya uhalifu, sambamba na matakwa ya kisheria. Angalia pia nyongeza ya “Fursa Sawa ya Ajira ni Sheria”, “EEO ni Sheria” na “Sharti la Kutobagua Uwazi wa Malipo.” Ikiwa una ulemavu au hitaji maalumu ambalo linahitaji kushughulikiwa, tafadhali tufahamishe kwa kujaza fomu hii.
DEI na maisha katika Uber
Angalia ukurasa wetu wa kazi ili upate taarifa zaidi kuhusu jinsi ilivyo kufanya kazi kwenye Uber.
Kuhusu