Mbinu: jinsi tunavyokadiria uepukaji wa uzalishaji wa gesi chafu
Hapa Uber, tunalenga kuwa wazi katika maendeleo yetu tunavyopiga hatua ili kuwa mfumo usioozalisha gesi chafu kabisa Hii ni pamoja na kuwa wazi kuhusu mbinu tunayotumia katika ukokotaji wetu. Kwa sababu hiyo, hati hii inatoa muhtasari wa jinsi tunavyokadiria uzalishaji wa gesi chafu kwa kila safari na uzalishaji unaoepukika kutokana na chaguo fulani za usafiri.
Upeo wa uzalishaji wa gesi chafu
Tunakadiria gesi ya CO₂ iliyozalishwa kutoka kwa bomba la moshi kuanzia wakati tunapomchukua msafiri hadi mwisho wa safari. Kwa sababu wasafiri hawana udhibiti wa umbali ambao madereva wanasafiri, tunalenga tu umbali wa safari. Hatujumuishi uzalishaji usio wa bomba la moshi, kama vile wa magari yanayosafirisha petroli hadi vituo vya mafuta, kwa sababu ushawishi wa Uber kuhusu uzalishaji wa hewa chafu kama huo ni mdogo mno. Katika sekta ya usafiri, CO₂ inachangia asilimia 99 ya gesi joto inayotokana na uchomaji wa nishati inayotokana na visukuku (GHGs), kwa hivyo, ili kufanya iwe rahisi, tunaondoa gesi zisizo za CO₂ GHGs katika ukokotaji wetu.
Uzalishaji wa gesi chafu kwa kila safari
Tunakadiria uzallishaji wa gesi chafu kwa kila safari kulingana na (1) wastani wa uzalishaji wa gesi chafu kwa kila maili ya gari la kawaida katika chaguo la usafiri (km Uber Green) na (2) umbali uliosafiriwa. Mbinu hii huturuhusu kukadiria hali zinazofaa za kubuni.
Wastani wa uzalishaji wa gesi chafu kwa kila maili hukadiriwa kwa kutumia mbinu ya Ripoti ya Tathmini ya Hali ya Hewa na Utendaji ya Uber mara nyingi iwezekanavyo. Kwa mfano tukiwa na Namba ya Utambulisho wa Gari (VIN), tunatumia maelezo hayo kupata data ya kina zaidi ya uzalishaji wa gesi chafu. Wakati mbinu ya CAsPR haitoshi kutambua tofauti kati ya bidhaa za kawaida na bidhaa zinazotoa kiwango cha chini cha gesi chafu (hasa nje ya Marekani/Kanada/Ulaya), tunatumia rekodi za safari za gari kukadiria aina ya mafuta na injini ya magari. Kwa mfano, gari lililokamilisha angalau safari 10 za Comfort Electric huchukuliwa kuwa gari la umeme, ilhali gari lililokamilisha angalau safari 10 za Uber Green huchukuliwa kuwa mahuluti. Tunapotambua aina ya injini kuwa ya seli ya umeme, betri au mafuta, tunachukulia kuwa hakuna uzalishaji wa gesi chafu. Kwa magari mahuluti, tunachukulia kuwa uzalishaji wa gesi chafu umepungua kwa asilimia 33 ikilinganishwa na magari ya kawaida yanayotumia mafuta. Kumbuka kuwa tunapokadiria uzalishaji wa gesi chafu, tunazingatia vipengele vingine kama vile mchanganyiko wa magari, ambao huturuhusu kuakisi kwa usahihi zaidi kwamba Uber Green na pia UberX zinajumuisha magari ya umeme na mahuluti.
Umbali unaozingatiwa hukadiriwa kulingana na pointi za GPS. Tunatumia mbinu ya kulinganisha ramani ili kupunguza athari za hitilafu ya data ya GPS.
Ukadiriaji wa uepukaji wa uzalishaji wa gesi chafu
“Uepukaji” wa uzalishaji wa hewa ya ukaa unawakilisha uzalishaji wa hewa ya ukaa ambao msafiri ameepuka kwa kuomba moja kwa moja aina ya usafiri wa kiwango cha chini cha uzalishaji wa hewa ya ukaa. Uepukaji wa uzalishaji wa hewa ya ukaa huhesabiwa kama tofauti ya kaboni dioksidi inayotokana na aina za usafiri za kiwango cha chini cha uzalishaji wa hewa ya ukaa kwenye programu ya Uber na zile za programu nyingine zenye uzalishaji wa hewa ya ukaa wa kawaida. Kwa hivyo, kwa mfano, uzalishaji wa hewa ya ukaa kutoka kwenye safari za Uber Green, UberX Share (pia inajulikana kama Pool) na magari madogo hulinganishwa na ule wa safari za UberX na uzalishaji wa hewa ya ukaa wa Comfort Electric hulinganishwa na uzalishaji wa hewa ya ukaa wa Uber Comfort. Wakati UberX au Comfort hazipatikani sokoni, tunachagua huduma inayofanana zaidi kulingana na bei na umaarufu. Kwa UberX Share (pia inajulikana kama Pool), tunahesabu tu safari zinazolingana na wasafiri wengine na tunakadiria uepukaji wa uzalishaji wa hewa chafu kwa kulinganisha safari za pamoja na safari za moja kwa moja. Umbali uliosafirishwa wakati wa safari za pamoja unagawanywa kati ya idadi ya vikundi vya msafiri. Kwa aina zote za usafiri, hatuhesabu uepukaji wa uzalishaji wa hewa ya ukaa kwa safari zilizo chini ya kilomita 1.
Maelezo zaidi
Kwa sababu kiwango cha wastani cha uzalishaji wa hewa ya ukaa (gCO2 kwa kila maili au kilomita) cha aina ya usafiri hubadilika kadiri muda unavyopita na hutofautiana kulingana na mji, tunafanya hesabu hii kwa kila aina ya usafiri katika kila mji na kusasisha kila mwezi. Wakati hakuna safari za kutosha katika mji fulani ili kuhesabu wastani wa ufanisi wa uzalishaji wa hewa ya ukaa, tunatumia kiwango cha wastani cha ufanisi wa uzalishaji wa hewa ya ukaa katika aina hiyo ya usafiri.
Hesabu ya uepukaji wa uzalishaji wa hewa ya ukaa inategemea safari za msafiri tangu mwanzoni mwa mwaka 2021, isipokuwa Lime ambayo inaanza mwezi Julai, 2022. Ikiwa msafiri amekuwa mtumiaji baada ya mwezi Januari 2021, tunakadiria uokoaji wa pesa kulingana na safari zake tangu alipokuwa mtumiaji.
Katika matukio machache, safari za pamoja zinaweza kukosa kuzuia uzalishaji wa hewa chafu (km mzunguko wa safari za UberX Share (pia unajulikana kama Pool) ukiwa mrefu kuliko ilivyotarajiwa); uzalishaji wa hewa chafu hautajumlishwa katika hesabu ya jumla.
Kuhesabu ulinganifu
Ulinganifu hukokotolewa kama ifuatavyo:
- Matumizi ya mafuta: Tunafuata vipimo vya EPA ya Marekani vya uzalishaji wa gesi ya CO2 kutokana na petroli.
- Umbali unaoendeshwa kwenye gari linalotumia mafuta: Tunachukulia kuwa gari linasafiri maili 25.2 kwa galoni moja (mpg) ya petroli (wastani wa galoni ya mafuta yanayotumika kwa kila maili na magari ya kazi nyepesi nchini Marekani) na kufuata vipimo vya EPA ya Marekani vya uzalishaji wa gesi ya CO2 kutokana na mafuta ya petroli.
- Uchafu unaorejelezwa kuwa mpya badala ya kutupwa: Tunafuata makadirio ya EPA ya Marekani.
- Msitu huondoa CO2 kutoka angahewa kwa mwaka mmoja: Tunafuata makadirio ya EPA ya Marekani.
- Maili za usafiri kwenye safari ya ndege ya kimataifa: Tunafuata vigezo vya uzalishaji wa DEFRA vya Uingereza.
- Utumiaji wa makaa ya mawe: Tunafuata vipimo vya EPA ya Marekani vya uzalishaji wa gesi ya CO2 kutokana na makaa ya mawe.
- Fulana za mikono zinazotengenezwa: Tunafuata makadirio ya Taasisi ya Rasilimali Duniani ya fulana za mikono zinazotengenezwa kwa pamba.
Kuhusu