Huduma bora ya Uber kwa ajili ya biashara yako
Tovuti ya kusimamia safari za kimataifa, milo na usafirishaji wa bidhaa katika eneo husika kwa kampuni zenye ukubwa wowote.
Tovuti ya kimataifa kwa ajili ya mahitaji yako yote ya biashara
Safari
Safari za kwenda na kutoka kwenye uwanja wa ndege. Safari za kila siku. Safari kwa ajili ya wateja. Wakati biashara yako inahitaji kupiga hatua, unaweza kuomba safari katika zaidi ya miji 10,000 kote ulimwenguni.
Milo
Ni vigumu kufanya kazi nzuri ukiwa na njaa. Hakikisha kwamba wafanyakazi wako wana motisha na wageni wako wanapewa chakula cha kutosha kutoka kwa washirika wa mikahawa zaidi ya 780,000.
Kusafirisha bidhaa
Kwa vifurushi vyenye uzito wa chini ya pauni 50, kuanzia maagizo ya rejareja hadi bidhaa za magari, tunaweza kusaidia biashara yako iwafikie wateja kwa haraka zaidi kuliko hapo awali kupitia ufikiaji wa machaguo ya kusafirisha bidhaa ya siku hiyohiyo katika eneo lako.
Kwa nini utumie tovuti yetu
Fikia Uber kote ulimwenguni
Programu hii inapatikana katika zaidi ya nchi 70 na miji 10,000 kwa hivyo huduma yetu inawashughulikia wafanyakazi wako wanapokwenda kazini.
Punguza na udhibiti matumizi
Unaweza kuunda mipango ya usafiri na milo inayolingana na bajeti yako. Isitoshe, unaweza kupata ripoti na vidokezi kupitia dashibodi rahisi.
Uupe usalama kipaumbele
Utaratibu wetu mpya wa Usalama Unapotoka Sehemu Moja hadi Nyingine umebuniwa ili kulinda afya na usalama wa kila mtu anayetumia tovuti yetu.
Wafurahishe wafanyakazi wako
Wawezeshe wafanyakazi na wateja wafikie tovuti inayotumiwa na mamilioni ya watu.
Jiunge na zaidi ya kampuni 150,000 zinazofanya kazi pamoja nasi, ikiwemo zaidi ya nusu ya idadi ya kampuni zilizo kwenye Fortune 500
Wakati Zoom, ambayo ni kampuni inayoongoza katika mikutano ya video ilipoanza kuimarika kote ulimwenguni, Uber ilipiga hatua pamoja nayo ili kuwasaidia wafanyakazi wake kupata magari wanapotaka kusafiri kote ulimwenguni.
Wakati wafanyakazi walianza kufanya kazi wakiwa nyumbani, Kampuni ya Coca-Cola ilitoa vocha za Uber Eats ili kusaidia kuongeza motisha ya wafanyakazi na kusaidia migahawa ya eneo husika.
Samsung Canada iliongeza mauzo ya vifaa vya mkononi vya Galaxy kwa asilimia 20 kwa kuwapa wateja vocha za Uber Eats za USD100.
Biashara yako inazidi kuimarika. Tuko hapa ili kukusaidia.
Muhtasari
Kutuhusu
Huduma
Huduma
Kulingana na matumizi
Kulingana na tasnia
Usaidizi kwa wateja
Usaidizi
Nyenzo
Pata maelezo