Usalama na heshima kwa wote
Mwongozo wa Jumuiya ya Uber
Tumebuni mwongozo wetu ili kufanya kila huduma iwe salama, iheshimike na iridhishe.
Kila mtu anayejisajili katika akaunti ya Uber kwenye programu zetu zote, ikijumuisha, lakini si tu kwa madereva, wasafiri, wasafirishaji wa bidhaa, watumiaji wa Uber Eats, wauzaji na watumiaji wa JUMP, anatarajiwa kufuata mwongozo huu
Mwongozo katika kifungu hiki husaidia kukuza uhusiano mzuri kwenye jumuiya yetu pana wakati wowote wa huduma.
Timu yetu inajitahidi kila siku ili kuwezesha huduma salama kwa kila mtu. Vigezo hivi vilitungwa kwa sababu hili. Unaweza pia kupata mwongozo mahususi wa Uber Eats katika sehemu hii.
Tumejitolea kufuata sheria. Tunatarajia watumiaji wote wa App zetu watekeleze wajibu wao kwa kutii sheria husika.
Mwongozo wa ziada kwa Uber Eats
Pamoja na kufuata Mwongozo wa Jumuiya ya Uber, angalia vigezo vyetu vya oda na usafirishaji wa Uber Eats.
Uwezo wa chaguo zako
Mamilioni ya watu wanafurahia huduma za Uber kila siku. Mahusiano haya mazuri husaidia kubainisha sifa yetu. Asante kwa kusaidia kufanya Uber kuwa jumuiya salama na changamfu.
Maoni yako ni muhimu
Tumekurahisishia mchakato wa kuripoti jambo likitokea, liwe nzuri au baya. Timu yetu inaendelea kuboresha viwango vyetu na maoni yako yanatusaidia kuchukua hatua inayofaa na kudumisha ufaafu wa viwango vyetu kadri teknolojia yetu inavyoimarika.
Ikiwa ungependa kuripoti tukio, tembelea help.uber.com au uwasiliane nasi kupitia App. Ukijipata hatarini, wasiliana na serikali ya eneo lako kabla ya kufahamisha Uber.
Ukadiriaji wa juu ni ushahidi kuwa unaendelea vizuri. Ikiwa tathmini yako iko chini ya wastani, idhini yako ya kufikia App huenda ikaondolewa kabisa au kwa muda. Idhini yako ya kufikia akaunti ikiondolewa kwa sababu ya tathmini zako, huenda tukashiriki maelezo yanayoweza kukusaidia kuboresha tathmini.
Uber hukagua ripoti zote zinazotumwa kwa timu yetu ya usaidizi ambazo huenda zinakiuka Mwongozo wetu wa Jumuiya na tunaweza kuchunguza kupitia timu maalum. Akaunti yako inaweza kusimamishwa hadi tutakapokamilisha ukaguzi wetu. Ukiukaji wa mwongozo wetu wowote unaweza kusababisha kuondolewa kwa idhini yako ya kufikia akaunti za Uber.
Ukurasa huu unatumika kama nyenzo ya kutoa muhtasari wa Mwongozo wa Jumuiya ya Uber. Ili usome kwa kina Mwongozo wetu wa Jumuiya, nenda hapa upate mwongozo husika wa Ulaya na Afrika Kusini mwa Sahara na sehemu hii ili upate mwongozo husika wa Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini. Madereva na watumiaji wa Uber Eats wanaweza kupata sheria na masharti ya Uber na Uber Eats hapa na sheria na masharti ya baiskeli za JUMP hapa. Washirika wanaweza kupata mkataba wao wa kisheria na Uber hapa.
Ukiukaji wa Mwongozo wetu wowote wa Jumuiya unaweza kusababisha kuondolewa kwa idhini yako ya kufikia akaunti zako za Uber. Huenda hali hii ikajumuisha hatua kadhaa unazoweza kuchukua nje ya App, ikiwa tutabaini kuwa vitendo hivyo vinatishia usalama wa jumuiya ya Uber, wafanyikazi wetu na watoa huduma au kusababisha madhara kwa chapa, hadhi au biashara ya Uber.
Kuhusu