Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Fuata sheria

Sehemu hii inategemea sheria na kanuni ambazo kila mtu lazima azifuate. Kwa mfano, haikubaliwi hata kidogo kutumia app za Uber kutenda au kujaribu kutenda uhalifu wowote au kukiuka sheria au kanuni yoyote.

Viti vya watoto

Madereva na wasafiri wanapaswa kufuata sheria za nchi husika wanaposafiri na watoto wachanga na watoto wadogo. Ni wajibu wa msafiri aliye na mtoto kutoa na kuweka kiti cha gari kinachofaa isipokuwa sheria ibaini vinginevyo.

  • Unaposafiri na watoto wadogo, ni jukumu lako kuweka kiti cha gari isipokuwa sheria ibaini vinginevyo.

  • Unapowachukua watu wanaosafiri na watoto wadogo, huenda utahitaji kuchukua muda zaidi kuweka kiti cha mtoto vizuri kabla ya kuanza kuendesha gari.

Fuata sheria zote

Una jukumu la kufahamu na kutii sheria na kanuni zote zinazotumika wakati wote unapotumia app za Uber. Hii ni pamoja na sheria na kanuni za uwanja wa ndege na sheria za barabara, kama vile sheria kuhusu kasi na za foleni barabarani.

  • Leseni zote husika, vibali, na hati zingine zozote za kisheria zinazohitajika kwa madereva na matarishi sharti ziwe zinatumika. Kwa mfano, madereva na matarishi wote wanaotumia gari wanahitajika kisheria kuwa na leseni na bima halali ya dereva. Madereva lazima pia wakidhi masharti ya kisheria katika eneo lako. Tunakagua ripoti za ajali na makosa ya trafiki ambayo yanaweza kutokea wakati wa kusafirisha mizigo au watu. Sheria za nchini zinazohusu maegesho zinaweza kukuzuia kuegesha gari katika baadhi ya maeneo unapochukua oda, kusafirisha mizigo, kusubiri wasafiri wawasili, au kurudisha baiskeli, mopedi au skuta iliyokodishwa kupitia app za Uber. Kwa mfano, ni kinyume cha sheria kufunga njia za baiskeli au kufunga njia za walio na ulemavu.

  • Kwa usalama wa kila mtu, mwache dereva au tarishi amakinikie kuendesha gari. Usiguse usukani, kwa mfano, au gia au vinundu, vitufe au vifaa vingine ambavyo vinatumika kuendesha gari. Usimweleze dereva au tarishi kuongeza kasi au kusimama, kushukisha au kupitia mahali pasiporuhusiwa.

  • Unapoendesha au kuegesha baiskeli, mopedi au skuta kupita app ya Uber, fuata sheria na kanuni za nchini; unaweza kurejelea tovuti ya serikali yako au ya mamlaka ya mtaa uone sheria zinazotumika. Kufuata sheria za barabarani kawaida hukuhitaji uwapishe watu wanaotembea kwa miguu, kuendesha upande wa waendesha magari wengine, kuonyesha ishara ikiwa unanuia kubadilisha mwelekeo, na kusimama kabisa kwenye taa nyekundu na alama za kusimama.

Wanyama wa kutoa huduma

Madereva sharti wampe usafiri abiria aliye na mnyama yeyote anayetoa huduma, kwa mujibu wa sheria, hata kama dereva ana imani tofauti za kidini au huwaogopa wanyama.

  • Kukataa maksudi kumsafirisha mtu kwa sababu ana mnyama wa kutoa huduma kutasababisha kupoteza uwezo wa kufikia app za Uber isipokuwa panaporuhusiwa kisheria.

Pombe na dawa za kulevya

Wasafiri wanakatazwa kubeba chupa za pombe zilizofunguliwa, au kuwa wamelewa wakisafiri kwenye safari.

  • Usiwahi kubeba ndani ya gari dawa haramu au chupa za pombe zilizofunguliwa. Ikiwa una sababu ya kuamini kuwa dereva wako ni mlevi au ametumia dawa za kulevya, mwambie aghairi safari hiyo mara moja. Kisha shuka na upige simu kwa mamlaka ya karibu au huduma za dharura. Ukishuka gari lako, tafadhali pia ripoti kuhusu tukio lako kwa Uber.

  • Kwa mujibu wa sheria, huwezi kuendesha gari au baiskeli ukiwa mlevi. Sheria haikuruhusu kuendesha gari au baiskeli ukiwa umekunywa pombe, dawa za kulevya au bidhaa nyingine kupita kiasi kinachoruhusiwa kisheria, hali ambayo inapunguza uwezo wako wa kuendesha gari kwa njia salama.

    Wasafiri wanakatazwa kubeba chupa za pombe zilizofunguliwa au kuwa wamelewa wakisafiri. Ukikumbana na msafiri aliyelewa kupita kiasi au mwenye vurugu, una haki ya kukataa safari kwa sababu ya usalama wako.

  • Usiwahi kusafiri ukiwa umekunywa pombe kupita kiasi kinachoruhusiwa kisheria, za kulevya dawa au bidhaa nyingine yoyote ambayo inapunguza uwezo wako wa kuendesha baiskeli, baiskeli mopedi au skuta kwa njia salama.

Bunduki

Wasafiri na wageni wao, na pia madereva, matarishi na watumiaji wa JUMP, hawaruhusiwi kubeba silaha za aina yoyote wanapotumia App za Uber, kwa kiwango kinachoruhusiwa na sheria husika.

Ulaghai

Udanganyifu unaweza kuvunja uaminifu na pia ni hatari. Hairuhusiwi kutoa maelezo ya uongo kwa makusudi au kutumia utambulisho wa mtu mwingine (au kumruhusu mtu mwingine kutumia utambulisho wako), kwa mfano wakati wa kuingia katika akaunti au kufanyiwa ukaguzi wa usalama.

Toa maelezo sahihi unaporipoti matukio, kufungua na kutumia akaunti zako za Uber, kupinga matozo au ada na kuomba mikopo. Omba tu ada, matozo au kurejeshewa pesa unakostahiki, na utumie ofa na matangazo tu kama ilivyokusudiwa. Usifanye mialama isiyo sahihi kimakusudi.

Shughuli zisizokubalika

Usiwahi kuomba au kukubali malipo nje ya mfumo wa Uber, isipokuwa ikiwa msafiri au mtumiaji wa Uber anatumia chaguo ya kulipa kwa pesa taslimu kwa usaidizi wa Uber.

Usiwahi kuharibu sifa za biashara au kampuni kwa kufanya mambo kama vile kutumia chapa au hakimiliki ya Uber bila ruhusa.

  • Madereva na matarishi wanapaswa kutumia tu bidhaa za Uber zilizopigwa chapa ambazo zinatolewa au kuruhusiwa na Uber. Matumizi ya bidhaa za kampuni nyingine ambazo haziruhusiwi—kama vile taa, mabango, ishara au bidhaa sawa na hizi zenye jina la Uber au alama yake ya biashara—zinaweza kuwachanganya wasafiri au watumiaji wa Uber Eats.

Angalia Miongozo zaidi ya Jumuiya

Heshimu watu wote

Tushirikiane kuimarisha usalama wa kila mtu