Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Heshimu watu wote

Tunaamini kuwa kila mtu anapaswa kuheshimiwa. Ndiyo sababu tumeweka kanuni za kudhibiti kugusana kimwili, dhuluma za kingono na matendo mabaya, vitisho na ujeuri, kugusana kusikotakiwa, ubaguzi na uharibifu wa mali.

Kugusana kimwili

Usimguse mtu usiyemfahamu au mtu yeyote ambaye umekutana naye unapotumia App yoyote ya Uber. Hairuhusiwi kamwe kumjeruhi au kupanga kumjeruhi mtu yeyote.

Dhuluma za kimapenzi na kukosea heshima

Dhuluma za kingono na matendo mabaya ya aina yoyote yamepigwa marufuku. Dhuluma za kingono na matendo mabaya yanarejelea kumgusa mtu kingono au kumfanyia jambo la kingono bila idhini ya wazi ya mtu huyo.

Nafasi ya kibinafsi na faragha inapaswa kuheshimiwa. Orodha ifuatayo inatoa mifano ya baadhi ya matendo yasiyofaa, lakini haijakamilika.

  • Tabia na matamshi ambayo yanaweza kuwakera watu hayakubaliki. Mifano inajumuisha kumdukua mtu, kumpigia mluzi au kumkonyezea macho. Usimguse au kumfanyia utani mtu usiyemfahamu.
  • Baadhi ya matamshi ambayo yanaweza kuonekana ya kawaida yanaweza kukera. Usitoe maoni kuhusu mwonekano wa mtu, utambulisho wa kijinsia au mwelekeo wake wa kingono. Usimuulize maswali ya kibinafsi yasiyofaa, kama vile, "Je, una mpenzi?" Usijadili maisha yako ya kingono au ya mtu mwingine, kutumia lugha chafu au kutania masuala ya ngono.
  • Uber ina kanuni inayokataza kabisa masuala ya ngono kazini. Ni marufuku kugusana kimapenzi wakati unatumia App za Uber, ikijumuisha wakati wa unasafirisha watu au chakula. Pata maelezo zaidi hapa.

Vitisho na matendo ya ujeuri

Matendo ya fujo, majibizano au unyanyasaji hayaruhusiwi. Usitumie lugha au ishara ambazo zinaweza kumkosea mtu heshima, kumtisha au zisizomfaa. Unashauriwa kutozungumzia mada za kibinafsi ambazo zinaweza kusababisha upinzani, kama vile dini na imani za kisiasa.

  • Tumia mazungumzo ya kawaida na ya kuchangamsha kwa matarishi, madereva, wauzaji na wasafiri wenza. Usiulize maswali ya kibinafsi au kuzua fujo dhidi ya watu wengine.

  • Tumia mazungumzo ya kawaida na ya kuchangamsha kwa watumiaji wa Uber Eats, wasafiri, wauzaji na watu wengine. Usiulize maswali ya kibinafsi au kuzua fujo dhidi ya watu wengine.

Mawasiliano yasiyotakikana

Mawasiliano yanapaswa kuisha wakati usafirishaji watu au chakula umekamilika, isipokuwa wakati wa kurudisha kitu kilichopotea au ikiwa kuna makubaliano kati ya wahusika wote wawili. Kwa mfano, hairuhusiwi kumtumia ujumbe mfupi, kumpigia simu, kuwasiliana katika mitandao ya kijamii, kumtembelea au kujaribu kumtembelea mtu binafsi baada ya usafirishaji wa abiria au chakula.

  • Unapaswa kuwasiliana na Uber haraka iwezekanavyo ikiwa mtumiaji wa Uber Eats, msafiri au muuzaji atawasiliana nawe bila kukubaliana nyote wawili kwa sababu yoyote ile isipokuwa kuhusu safari yako ya sasa au kusafirishiwa chakula au kurudishiwa kitu kilichopotea.

  • Wasiliana na Uber haraka iwezekanavyo ikiwa dereva au tarishi atawasiliana nawe bila kukubaliana nyote wawili kwa sababu yoyote ile isipokuwa kuhusu safari yako ya sasa au kusafirishiwa chakula au kurudishiwa kitu kilichopotea

Ubaguzi

Unapaswa kuhisi salama na kuheshimiwa kila wakati. Ndiyo maana haturuhusu matendo tunayotaja kuwa ya ubaguzi. Usimbague mtu kwa msingi wa sifa kama vile umri, rangi, ulemavu, utambulisho wa kijinsia, hali ya ndoa, asili ya kitaifa, rangi, dini, jinsia, mwelekeo wa kijinsia au sifa zozote zinazolindwa kwa mujibu wa sheria husika. Haikubaliki pia kumtathmini mtumiaji mwingine, iwe ni mtumiaji wa Uber Eats, tarishi, dereva, muuzaji au msafiri, kwa msingi wa sifa hizi.

  • Hairuhusiwi kukataa au kughairi oda kwa sababu ya sifa zilizolindwa kisheria za mtumiaji au tarishi wa Uber Eats. Ikiwa unaamini tarishi anakataa kuchukua kitu kwa sababu ya sifa zako au za watumiaji wa Uber Eats zilizolindwa kisheria, tafadhali ripoti tukio hilo kwenye App ya Uber.

  • Ikiwa unaamini umenyimwa usafiri au kusafirishiwa mizigo kwa sababu ya sifa zako zinazolindwa kisheria, tafadhali ripoti tukio hilo kwenye App ya Uber.

  • Unapoendesha baiskeli au kusafiri kupitia App za Uber, ikiwa unaamini kuwa mtumiaji mwingine amekunyanyasa, kukutukana au kukudhulumu kwa msingi wa sifa zako zinazolindwa kisheria, tafadhali ripoti tukio hilo kwenye App ya Uber.

Kuharibu mali na kufunga vyombo vya usafiri

Hairuhusiwi kamwe kuharibu mali. Baadhi ya mifano inajumuisha kuharibu gari, baiskeli, baiskeli yenye injini, pikipiki au chombo kingine cha usafiri ulichoomba kupitia App za Uber; kuvunja au kuharibu simu au tableti; kumwaga chakula au kinywaji kimakusudi ndani ya gari; kuvutia sigara kwenye gari; au kutapika kwa sababu ya ulevi au vinginevyo. Ukiharibu mali, utawajibikia gharama ya kuisafisha na kuikarabati, bila kujumuisha uharibifu wa kawaida unaosababishwa na matumizi.

Ukikodisha baiskeli, baiskeli yenye injini au skuta kupitia App za Uber, sharti uhakikishe imefungwa salama mwisho wa safari yako. Kukosa kufanya hivyo kunaweza kusababisha utozwe gharama au ada ya ziada.