Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Kuwashukuru madereva wote na watu wanaosafirisha bidhaa

Maelfu ya madereva na watu wanaosafirisha bidhaa waliendelea kusafirisha bidhaa muhimu wakati wa janga la ugonjwa.

Wasafiri na wateja wa kusafirisha chakula mara kwa mara hushiriki shukrani zao ulimwenguni kote na madereva na watu wa kusafirisha bidhaa. Tulihuisha mazungumzo haya kupitia michoro ya ukutani ili kuonyesha baadhi ya madereva na watu wanaosafirisha bidhaa wakibadilisha hali mbalimbali kote ulimwenguni.

Kristin, Florida, Marekani

Andrew, msafiri ambaye alikuwa likizoni huko Florida, alikutana na Kristin muda mfupi baada ya maji ya mfuko wa mimba wa mkewe Suzanne kuvuja karibu katikati ya ujauzito wake.

Kristin alimwendesha kwenda kwenye kituo cha kufulia nguo ili afue nguo. Andrew alimsimulia hadithi yake na badala ya hii kuwa safari moja tu, Kristin alifanya zaidi ya vile alivyotarajiwa. Alikuwa mtu wa kutegemewa kwa wanandoa hao wakati Suzanne alikuwa hospitalini, akipeleka chakula kilichopikwa nyumbani na chochote ambacho wanandoa hao walihitaji. "Alitushughulikia katika ukaaji wetu hospitalini kwa wiki 10," Andrew anasema.

"Nadhani Kristin ni mtu mwenye fadhili na mkarimu zaidi kuliko wote niliowahi kukutana nao maishani mwangu." —Andrew, msafiri

Michelle, Manchester, Uingereza

Michelle ni tarishi huko Manchester, Uingereza. Kama mama na mzazi mlezi anayewalea watoto 5, anapenda kutumia Programu ya Dereva kama "wakati wa kupumzika akiwa mwenyewe" ili kutoka nyumbani na kuwaona watu wengine. "Wakati shughuli zilisitishwa kimataifa, nimekuwa na wateja wengi wazee," anasema. “Ninaacha chakula mlangoni na ninasimama na kuwasubiri wakichukue. Na wanapenda kupiga gumzo kidogo, labda kwa sababu hawajamwona mtu yeyote. Hivyo ndivyo ninavyofanya: Ninasimama na kupiga gumzo.”

Haiba ya uchangamfu na tabia ya kupenda kupiga gumzo ya Michelle imewafurahisha watu kote Manchester anapopeleka chakula mlangoni mwao. Asante, Michelle.

Jaswinder, Chandigarh, India

Jaswinder anachanganya kazi kwenye shamba la familia yake na kuendesha gari na Uber. Na ameendesha gari kwa safari 32,000, idadi kubwa zaidi kwa dereva yeyote nchini India, kwa miaka 5 ambayo amekuwa dereva. Kwa kutumia Programu ya Dereva, ameweza kushughulikia gharama na kuunda mtindo mzuri wa maisha kwa ajili ya familia yake. "Kuendesha gari kupitia Uber hunipa fahari," anasema. "Ninaendesha gari kwa masharti yangu mwenyewe na ninaendesha biashara yangu mwenyewe." Asante, Jaswinder.

"Kuendesha gari kupitia Uber hunipa fahari," anasema Jaswinder. "Ninaendesha gari kwa masharti yangu mwenyewe na ninaendesha biashara yangu mwenyewe."

Kristin, Michelle, na Jaswinder ni mifano michache tu ya watu wanaoendesha gari na kusafirisha bidhaa kupitia Uber ambao wameunda kumbukumbu za kudumu kwa ajili ya wengine kupitia mwingiliano wao wa kila siku. Kwa muda fulani, picha zao za ukutani zilikuwa kwenye pande za majengo huko New York, London na Manchester. Kwa muda mrefu zaidi, asante zitaendelea kusemwa kote ulimwenguni.

Je, kuna dereva au mtu anayesafirisha bidhaa ambaye ungependa kumshukuru? Teua Shujaa wako wa Kila Siku hapa.

Soma zaidi kuhusu kazi yetu yenye matokeo

Ahadi zetu

Kufanya usafiri kuwa sawa kwa ajili ya wote.

Biashara za Watu Weusi ni muhimu

Kusaidia biashara za Watu Weusi kote ulimwenguni.

Njia bora ya kufanya kazi

Kuwasaidia madereva na watu wanaosafirisha bidhaa kote ulimwenguni ili kuwasaidia kufanikisha malengo yao.