Please enable Javascript
Ruka uende katika maudhui ya msingi

Tunajivunia zaidi ukituamini

Kanuni za Faragha za Uber

Unapotumia huduma za Uber, una imani kwamba tutalinda data yako ya binafsi. Tumejizatiti kudumisha uaminifu huo na hiyo inaanza na kukusaidia kuelewa desturi zetu za faragha. Kanuni zetu za Faragha huweka msingi wa jinsi tunavyoshughulikia faragha hapa Uber.

Tunaifanyia data mambo yanayofaa.

Usimamizi wa data kwa kuwajibika ni sharti la uvumbuzi endelevu. Tunadumisha thamani ya data binafsi kwa ajili ya Uber na watumiaji wetu kwa kushughulikia data kulingana na matarajio ya watumiaji, tukiitunza ikiwa sahihi na iliyokamilika na kuiharibu ipasavyo pale inapokuwa haihitajiki tena. Hii huboresha huduma zetu, huwafanya watumiaji wetu watuamini na hututofautisha sokoni.

Tunaunda faragha kwenye bidhaa zetu kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Faragha ni kipengele muhimu cha kuunda bidhaa na huduma za kiwango cha kimataifa, kuanzia uanzishaji hadi uzinduzi na kuendelea. Kufanya ukaguzi wa faragha kwenye bidhaa, teknolojia na huduma mpya na zilizobadilishwa huhakikisha kwamba zinatimiza matarajio ya watumiaji na kuunda msingi wa kuwapa wateja huduma ya kipekee. Hii inaitwa "faragha kwa makusudi."

Tunakusanya tu kile tunachohitaji.

Tunazingatia lengo mahususi tunapokusanya, tunapotumia au kushughulikia data binafsi ambalo linalingana na malengo na maadili yetu. Tunakusanya na kutumia tu kiasi cha data binafsi tunayohitaji kwa makusudi halali na yaliyoidhinishwa.

Tuna uwazi kuhusu desturi zetu za data.

Tunasema waziwazi kuhusu data binafsi tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia na kuishiriki. Tunafanya kile tunachosema.

Tunawapa watumiaji machaguo kuhusu data zao.

Tunawapa watumiaji machaguo dhahiri kuhusu faragha na vidhibiti vyao ambavyo ni rahisi kutumia ili waweze kusimamia data zao.

Tunalinda data binafsi.

Tunatoa ulinzi unaofaa na bora ili kuzuia kupotea, na utumiaji au ufichuaji usioidhinishwa wa data ya binafsi.

Dhibiti faragha yako

Tembelea Kituo chetu cha Faragha ili kufanya chaguo kuhusu jinsi tunavyotumia data yako, kuchunguza bidhaa za faragha na kudhibiti mipangilio yako ya faragha.

Jinsi tunavyotumia taarifa yako

Uber inaweka huduma za usafiri, usafirishaji wa chakula na huduma nyingine panapoweza kupatikana kwa urahisi. Kuelewa ni data gani tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia kunapaswa kuwa jambo rahisi.

Ilani yetuya Faragha inaelezea kwa kina data tunayokusanya na jinsi tunavyoitumia ili kukupa huduma salama na ya kuaminika ya mtumiaji.

Tumefupisha maelezo haya katika chati zilizo hapa chini kwa kila aina ya watumiaji wa Uber, hususan Wasafiri na Wapokeaji wa Oda na Madereva na Wasafirishaji wa Bidhaa.

Chati hizi pia zinaonyesha msingi wa kisheria ambao Uber hutegemea kwa kila utumiaji wa data chini ya sheria za faragha kama vile Kanuni ya Jumla ya Ulinzi wa Data ya Muungano wa Ulaya.

Unaweza pia kupakua toleo lililopanuliwa la chati hii.

Jinsi ya kusoma jedwali hili
  • ✓ inamaanisha kwamba tunatumia data hii kote ulimwenguni
  • ✓* inamaanisha kwamba tunatumia data hii kote ulimwenguni, isipokuwa katika Maeneo ya Kiuchumi ya Ulaya, Uingereza au Uswisi
  • Umuhimu wa Mkataba (CN)
  • Sababu Halali (LI)
  • Inajumuisha anwani, barua pepe, jina la kwanza na la mwisho, jina la kuingia, nenosiri, nambari ya simu, njia ya kulipa (ikiwa ni pamoja na maelezo yanayohusiana ya uthibitishaji wa malipo), picha ya wasifu, mipangilio (pamoja na mipangilio ya ufikiaji) na mapendeleo, na maelezo ya mpango wa uaminifu wa washirika wa Uber.

  • Inajumuisha maelezo yaliyowasilishwa wakati wa mchakato wa kutuma ombi la dereva/msafirishaji, kama vile historia ya dereva au rekodi ya uhalifu (panaporuhusiwa na sheria), hali ya leseni, majina maarufu na anwani za sasa na za awali, na haki ya kufanya kazi.

  • Inajumuisha tarehe ya kuzaliwa na/au umri ili kuthibitisha ustahiki wako wa kutumia bidhaa au huduma zilizowekewa vikwazo vya umri (kama vile Uber kwa vijana, au ukinunua pombe, tumbaku au bidhaa za bangi), na jinsia ili kuwezesha huduma au programu fulani (kama vile Mapendeleo ya Wasafiri Wanawake, uuzaji na matangazo), kupitia tafiti za hiari au kutoka kwenye data nyingine iliyokusanywa kutoka kwa watumiaji.

  • Ni pamoja na hati za utambulisho zilizotolewa na serikali, kama vile leseni za udereva au pasipoti (ambazo zinaweza kuwa na picha na nambari za utambulisho, tarehe ya mwisho wa matumizi, tarehe ya kuzaliwa na jinsia), na picha za kujipiga zilizowasilishwa na mtumiaji.

  • Inajumuisha kumbukumbu za gumzo na rekodi za simu, ukadiriaji au maoni, Orodha au hakiki za mikahawa au wafanyabiashara zilizoundwa na watumiaji, picha na rekodi zilizopakiwa, ikijumuisha rekodi za sauti za ndani ya programu.

  • Inajumuisha nafasi za kulala au kukodisha gari, saa na tarehe za safari ya ndege ijayo.

  • Inajumuisha data iliyokadiriwa au sahihi ya eneo.

  • Inajumuisha maelezo ya malipo (pamoja na kiasi kinachotozwa na njia ya malipo), uthibitisho wa kuwasilisha (ikiwa ni pamoja na picha au saini), maagizo maalum, mizio au mapendeleo ya chakula, takwimu zinazotokana na maelezo ya safari / oda ya awali (kama vile wastani, ada za kughairi, jumla ya safari / oda), maelezo ya safari au oda (pamoja na tarehe na saa, anwani zilizoombwa za maeneo ya kuchukuliwa na kukushushwa, umbali uliosafiri, jina la mgahawa au mfanyabiashara na eneo, bidhaa zilizoagizwa).

  • Inajumuisha maelezo yaliyokusanywa kuhusu usafiri au usafirishaji bidhaa, kama vile mapato, takwimu zinazotokana na maelezo ya awali ya usafiri/usafirishaji bidhaa (ikiwa ni pamoja na wastani, ada za kughairi, ada za kukubali, na jumla ya usafiri/usafirishaji bidhaa na maili ulizosafiri) na maelezo ya usafiri au usafirishaji bidhaa (pamoja na tarehe na saa, anwani za maeneo ya kuchukuliwa na kushushwa ulizoomba, umbali uliosafiri, jina la mgahawa au mfanyabiashara na eneo, na bidhaa zilizowasilishwa).

  • Ni pamoja na kuacha kufanya kazi kwa programu na shughuli nyingine za mfumo, tarehe na saa za kufikia, vipengele vya programu au kurasa zilizotazamwa na aina ya kivinjari.

  • Ni pamoja na vitambulishi vya kutangaza, data ya mwendo wa kifaa, anwani ya IP ya kifaa au vitambulishi vingine vya kipekee, miundo ya maunzi,, data ya mtandao wa simu, mifumo ya uendeshaji na matoleo na lugha unazopendelea.

  • Inajumuisha aina ya mawasiliano (simu au ujumbe wa maandishi), maudhui (ikiwa ni pamoja na rekodi za simu wakati tu watumiaji wanaarifiwa kuhusu rekodi hiyo mapema), na tarehe na saa.

  • Inajumuisha data inayoruhusu utambulisho kulingana na sifa za kimwili au za kibayolojia, kama vile maelezo ya uthibitishaji wa uso.

  • Inajumuisha kutoka kwa au kuhusiana na:

    • Maafisa wa kutekeleza sheria, wahudumu wa afya ya umma na mamlaka nyingine za serikali
    • Washirika wa mauzo na watoa huduma
    • Watoa huduma wanaosaidia kuthibitisha utambulisho au kugundua ulaghai
    • Wamiliki wa akaunti za Uber
    • Watoa huduma wa bima au magari
    • Kampuni za usafiri
    • Washirika wa biashara ya Uber (ufunguaji na ufikiaji wa akaunti, na API)
    • Washirika wa biashara ya Uber (kadi za malipo au mikopo)
    • Watumiaji au wengine wanaotoa maelezo kuhusiana na masuala ya usaidizi kwa wateja, madai au mizozo
    • Watumiaji wanaoshiriki katika programu za rufaa za Uber

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

  • Je, Uber hutumia vipi taarifa ya mahali nilipo?

    Tunaitumia ili kuwawezesha watumiaji wetu kuomba, kupokea au kutoa huduma za usafiri au usafirishaji bidhaa; kufuatilia na kushiriki hali ya safari; kuimarisha usalama na ulinzi wa watumiaji wetu; kwa utafiti na maendeleo; na kwa madhumuni mengine yaliyoelezwa katika Ilani yetu ya Faragha.

  • Je, Uber huonesha mtu mwingine maelezo yangu?

    Uber hushiriki data yako na wengine inapohitajika ili kuwezesha huduma unazoomba au kutoa kupitia Uber. Kwa mfano, ukiomba usafiri, tunashiriki jina lako la kwanza, ukadiriaji, mahali ulipoomba kuchukuliwa na kushushwa na dereva wako. Pia tunashiriki maelezo yako unapotumia vipengele vinavyohusisha kushiriki data, kama vile unaposhiriki safari yako au hali ya oda na marafiki au familia. Tunaweza pia kushiriki maelezo yako na washirika wetu wa biashara, kampuni tanzu watoa huduma na wabia wa biashara wa Uber au kuyaonesha kwa sababu za kisheria au iwapo kuna mzozo.

    Tazama Ilani yetu ya Faragha upate maelezo zaidi.

  • Je, maelezo yangu yatahifadhiwa kwa muda gani na Uber?

    Uber huhifadhi data yako kwa muda unaohitajika kwa madhumuni yaliyoelezwa katika Ilani yetu ya Faragha, ambayo hutofautiana kulingana na aina ya data, aina ya mtumiaji ambaye data inamhusu (mfano, wasafiri dhidi ya madereva), madhumuni ya data tuliyokusanya, na ikiwa ni lazima data ihifadhiwe baada ya ombi la kufuta akaunti kwa madhumuni yaliyoelezwa katika Ilani yetu ya Faragha.

    Kwa mfano, tunahifadhi baadhi ya data (kama vile data ya akaunti) kwa muda wa akaunti yako ya Uber ikihitajika ili kutoa huduma zetu. Data nyingine tunayohifadhi ilivyobainishwa inavyohitajika ili kukidhi mahitaji ya kodi, bima, kisheria au udhibiti (kwa mfano, tunahifadhi maelezo ya safari au oda kwa miaka 7).

  • Ni nini kitakachotendekea maelezo yangu ikiwa nitafuta akaunti yangu?

    Kufuatia ombi la kufuta akaunti, tunafuta akaunti na data yako, isipokuwa inapohitajika kwa madhumuni ya usalama, ulinzi, kuzuia ulaghai au kutii matakwa ya kisheria, au kwa sababu ya masuala yanayohusiana na akaunti yako (kama vile mkopo ambao haujalipwa au dai au mzozo ambao haujasuluhishwa). Ufutaji kama huo hufanyika ndani ya siku 90 baada ya ombi la kufutwa kwa wasafiri na wapokeaji wa oda na miaka 7 ya ombi la kufuta madereva na watu wanaosafirisha bidhaa, isipokuwa ikiwa ni muhimu kuhifadhi kwa sababu zilizo hapo juu.

  • Nitaombaje nakala ya data yangu?

    Unaweza kuomba nakala ya data yako hapa (unatakiwa kuingia katika akaunti). Tafadhali angalia hapa upate maelezo zaidi.

  • Je, ninawezaje kuwasilisha swali kwa Afisa wa Ulinzi wa Data wa Uber (DPO)?

    Afisa wa Uber Anayesimamia Usalama wa Data ana jukumu la kutuongoza kutii sheria ya ulinzi wa data katika Umoja wa Ulaya. Yeye huwaunganisha wasimamizi wa faragha Ulaya na masuala kuhusu faragha ya data kutoka kwa watumiaji. Unaweza kuwasilisha maswali kwa DPO yetu hapa.

1/6
1/3
1/2

Ili kupata maelezo zaidi, rejelea Angalizo la Faragha la Uber